Msanii maarufu wa filamu nchi Steven  mengele,’ Steve Nyerere’ amesema kuwa kupanda mlima Kilimanjaro sio kazi rahisi inampasa mtu kujipanga na kuwa na Afya iliyoimara

Hayo ni baada ya muigizaji huyo kushindwa kufiki kilele cha mlima huo kupitia kampeni ya Waziri wa maliasili na utalii Mh,Hamis Kingwangalla.

Steve ameeleza kuwa hofu na presha ndio sababu ya yeye kutoendelea na safari hiyo ya kuzikamilisha mita 5,895 za mlima Kilimanjaro, na kutahadharisha kuwa mlima Kilimanjaro sio mlimani City.

”Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kupanda mlima Kilimanjaro ambao kiuhalisia sio Mlimani City ni mlima wa kweli kabisa na mimi ni mtanzania mzalendo hivyo nilitaka nijionee mwenyewe, kiukweli kuna changamoto inabidi mtu ujiandae na nilijitahidi kwa kweli nimeishia Km 11, kuna wakati nilisikia presha, ulimi kutaka kutoka, unasikia pua zinatanuka yaani ni noma” amesema Steve Nyerere.

Aidha msanii huyo amesema safari ya twenzetu kilele katika mlima kilimanjaro ilidhamiriwa kukamilishwa na wasanii 25, lakini mpaka leo Octoba 2,2019 ni wasanii 6 pekee ndio waliofanikiwa kufika katika kille cha mlima huo akiwemo  mchekeshaji Ebitoke ,Dude na Single Mtambalike huku wasanii wengine wakiishia njaiani kutokana na madiliko ya hali ya hewa.

Video: Sister Fay afunguka hisia zake kwa Diamond ''mume bora kwangu''
Video: TAKUKURU kumulika ujenzi machinjio ya Vingunguti