Kiungo kutoka nchini Croatia na klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid Mateo Kovacic, huenda akatimkia Italia, baada ya uongozi wa klabu ya SSC Napoli kuonyesha nia ya kumsajili katika kipindi hiki cha dirisha la usajili.

Kovacic, ameingizwa kwenye mipango ya SSC Napoli kufuatia hitaji lake la kutaka kucheza kila juma, hali ambayo uongozi wa klabu hiyo ya mjini Naples huenda ikampata kwa urahisi.

SSC Napoli wameweka wazi mpango huo, na tayari wamethibitisha kuwa mbioni kutuma ofa ya usajili wa kiungo huyo mwenue umri wa miaka 24 wakati wowote baada ya fainali za kombe la dunia zinazoendelea nchini Urusi.

Hata hivyo huenda kukawa na changamoto ya kumng’oa Kovacic Santiago Barnabeu, kufuatia baadhi ya viipengele vilivyopo kwenye mkataba wa mchezaji huyo aliyejiunga na Real Madrid mwaka 2015, akitokea Inter Milan.

Mkataba wa sasa wa Kovacic unatarajiwa kufikia kikomo mwaka 2021, huku mara kadhaa aliyekua mkuu wa benchi la ufundi klabuni hapo Zinedine Zidane aliwahi kukataa kumuuza.

Mfaransa huyo aliyevunja mkataba wa kuendelea kukitumikia kikosi cha Real Madrid mwezi uliopita, alichukua maamuzi magumu ya kuwaruhusu wachezaji kama Morata, James na Pepe kuondoka, lakini ilipofika kwa Kovacic aligoma kufanya hivyo, kwa kisingizio cha kuamini kiungo huyo ni msaada mkubwa kikosini kwake, japo alikua hamtumii mara kwa mara.

Video: Wabunge waamsha 'dude' la korosho, Wabunge CCM wagawanyika
Video: Majaliwa kuzindua vituo 51 vya hali ya hewa vinavyojiendesha vyenyewe