Spika za masikioni zisizounganishwa na waya (waireless headphones), zimetajwa kuwa moja kati ya vyanzo vya ugonjwa hatari wa saratani, hii ni  kwa mujibu wa wataalamu wa afya 250 waliopeleka utafiti wao shirika la afya la kimataifa (WHO).

wataalamu hao wamesema vifaa hivyo vina mawimbi – radio aina ya electromagnetic frequency (EMF), ambayo huzalisha joto linaloathiri ukuaji wa chembe hai za damu katika mwili wa binadamu.

Wameeleza kuwa kinachowatia hofu zaidi ni ukaribu uliopo kati ya ‘Wireless’ hizo na fuvu la kichwa wakiamini kuwa inaweza kuwa na madhara kwa afya ya mtumiaji.

Profesa wa chuo kikuu cha Colorado, nchini Mearekani, Jerry Phillips, ambaye ni miongoni mwa wanasayansi hao amekiambia kituo cha televisheni cha Medium kuwa anahofu na madhara yanayoweza kutokea kwenye mishipa ya kichwa.

” Wasiwasi wangu ni kwamba, zinavyowekwa katika sikio, zinafanya mishipa ya kichwa kuwa karibu zaidi na mionzi” alisema.

Yeye pamoja na wenzie wameiomba WHO kusitisha maramoja matumizi ya teknolojia hiyo, ambapo katika waraka wao wanaeleza kuwa mbali ya saratani, mionzi ya spika hizo za ‘wireless’ inaharibu vinasaba (DNA) vya mtumiaji.

Zaidi ya watu milioni 28 ulimwenguni wanakadiriwa kuwa wanatumia teknolojia hiyo, huku biashara ikionekana kuwa nzuri kwa kampuni ya Apple, ambayo imejitetea na kusema kuwa wao vifaa vyao wanavitengeneza kwa kujali afya za watumiaji wao.

 

 

Cardi B kukumbwa na kashfa iliyomponza R Kelly
Waathirika wa VVU Songea waanzisha mradi wa ufugaji kuku