Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amesema kuwa kuna baadhi ya wabunge wanamsongo wa mawazo kwasababu ya madeni mbalimbali waliyokopa bungeni hapo.

Ameyasema bungeni jijini Dodoma alipotangaza deni analodaiwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambalo ni zaidi ya shilingi milioni 416 kuwa huenda ni sababu inayomfanya Mbunge huyo kutokuwa sawa.

Spika Ndugai ametangaza deni hilo katika muendelezo wa vikao vya Bunge Jijini Dodoma, wakati akielezea uamuzi wa kumtaka Mbunge Lema kufika kwenye kikao cha Kamati ya Maadili ya Bunge, kujibu madai ya kuunga mkono kauli ya kuwa Bunge ni ‘dhaifu’.

“Yapo mambo ambayo huwa hatuyasemi, ngoja tuseme kidogo, Lema amekopa milioni 644, sasa hivi ameshalipa milioni 200, huu ni msongo wa mawazo ndiyo maana anajilipua na kadhalika,”amesema Spika Ndugai

Aidha, akitangaza uamuzi wa kumtaka Lema kwenda Kamati ya Maadili Ndugai amemtaka afike kwenye kikao saa 8 mchana na kesho itakuwa hatma yake.

Hata hivyo, mapema jana Kamati ya Maadili, ilitangaza kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad na kutangaza kumsimamisha mikutano miwili Mbunge wa Kawe Halima Mdee.

Harmonize amvisha pete Sarah Italy
Pierre kupaa na Taifa Stars AFCON nchini Misri