Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa katika Uwakilishi wa Bunge la Afrika kumetokea matatizo makubwa hasa kwa Mhe.Steven Masele.

Amesema kuwa matatizo ni ya kinidhamu, hivyo wamelazimika kumrudisha nyumbani kuanzia jumatatu lakini badala yake amekuwa akionyesha kugoma kurudi nyumbani kwaajili kuhojiwa na kamati ya bunge ya maadili.

”Tumelazimika kumrudisha nyumbani kuanzia Jumatatu badala yake amekuwa akionyesha kugoma, ni kiongozi ambaye anafanya mambo ya hovyo hovyo ndo maana tumemuita kidogo kwenye kamati ya maadili ili atufafanulie,” amesema Spika Ndugai.

Ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma kabla ya kuanza kipindi cha maswali na majibu, ambapo amesema kuwa ameandika barua rasmi kwenye uongozi wa bunge hilo ili kuweza kumsimamisha kazi mbunge huyo.

Dada wa kazi aadhibiwa kwa kufungwa mtini siku 4
Iran yailaumu Marekani kwa kuchochea mvutano

Comments

comments