Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata Mbunge wa Jimbo la Kawe (CHADEMA) Halima Mdee.

Spika Ndugai ameagiza Mbunge huyo akamatwe ili kujibu tuhuma za kutoa lugha za matusi kwa Spika wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika April 4, 2017.

Aidha, Spika Ndugai amemtaka kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kufika katika kamati ya maadili, kinga na madaraka ya Bunge leo Aprili 6, 2017 kwa ajili ya kujibu tuhuma za kulidhalilisha Bunge.

Kama ilikupita hii: Bungeni Dodoma Kipindi cha Maswali na Majibu leo April 06, 2017

Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma
Hugo Broos Abadili Mawazo, Kuendelea Na Cameroon