Meneja wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amewatia moyo mashabiki na wachezaji wake baada ya kupokea kipigo cha 2-0 jana usiku kutoka kwa Paris Saint-Germain (PSG) wakiwa nyumbani.

Kipigo hicho cha magoli yaliyopatikana katika kipindi cha pili kupitia kwa Presnel Kimpembe na Kylian Mbappe kiliwapa PSG  nafasi zaidi ya uwezekano wa kuvuka ng’ambo ya mto wa ligi hiyo na kuwapa wakati mgumu wekundu wa Old Trafford.

Jaribio la kujiimarisha zaidi na kugeuza matokeo hayo lilikuwa gumu, na pigo lingine kwa Manchester United liliibuka dakika ya 89 baada ya Paul Pogba kulimwa kadi nyekundu.

Solskjaer ameonesha kutokuwa na wasiwasi na maendeleo ya kikosi chake, ikiwa ni mechi yake ya kwanza kwenye Ligi hiyo, amesema kuwa uzoefu ulikuwa chanzo kikuu.

“Unaweza kuona kuwa hatujawahi kucheza mechi ya kiwango hiki kwa muda mrefu na tunapaswa kujifunza kutokana na uzoefu huu, kwa sababu ilikuwa moja kati ya uzoefu ambao unaweza kusababisha matokeo yoyote. Haiwezi kutoa maana halisi ya msimu wetu, itakuwa ni mechi moja ambayo tunamejifunza kwayo,” Solskjaer amewaambia waandishi wa habari.

Amesisitiza kuwa hawajakata tamaa kwa kipigo cha nyumbani na kwamba watakwenda Parisi Ufaransa tena wakiwa na imani ya kupata ushindi dhidi ya PSG.

Katika hatua nyingine, meneja huyo amesema kuwa hivi sasa hawana muda wa kupoteza kutafuta lawama kwani wanaamini watapita, na wanajipanga kwa ajili ya Chelsea na Liverpool.

“Hatuna muda wa kupoteza, tuna mlima wa Chelsea na Liverpool mbele yetu. Tutakuwa tayari kwa Chelsea, msiwe na shaka kuhusu hilo,” alisema.

Ughaibuni: Mtanzania akamatwa na dawa za kulevya tumboni
Tanzia: Godzilla afariki dunia, chanzo cha kifo chake chatajwa