Meneja aliyepata mafanikio makubwa Old Trafford, Sir Alex Ferguson amezungumza kwa mara ya kwanza suala la mapendekezo ya uteuzi ya meneja aliyemuachia kijiti cha ukuu wa benchi la ufundi la Man Utd, David Moyes.

Ferguson, ambaye aliondoka Old Trafford mwaka 2013, amesema ni kweli alimpendekeza Moyes kuchukua mahala alipopaacha klabuni hapo na anaamini hakukosea kutoa pendekezo hilo kwa viongozi wa Man Utd.

Amesema alimjua na kumfahamu vizuri Moyes na hakuwa na shaka na utendajui wake wa kazi, ambao ulimridhisha tangu alipoanza kuwa mkuu wa benchi la ufundi mwaka 1998 akiwa na klabu ya Preston North End.

Ferguson aliyazungumza hayo usiku wa kuamkia hii leo alipokua akizindua kitabu chake kingine ambacho kinazungumzi maisha yake ya ndani na nje soka ambapo alisisitiza suala la kutolaumiwa kwa mapendekezo aliyowaachia viongozi wa Man Utd.

Amesema hakuwa mpuuzi wana mjinga kuwaacha mameneja waliokua wakipewa kipaumbe kwa kipindi hicho kama Pep Guardiola, Jose Mourinho, Jurgen Klopp pamoja na Carlo Ancelotti na kumuona Moyes anafaa kwa Man Utd.

Hata hivyo mzee huyo mwenye umri wa miaka 73, amesema anaamini Moyes hakupewa nafasi ya kutosha na alichukuliwa kama sehemu ya mafanikio aliyoyaacha klabuni hapo kitu ambacho kilikua sio sahihi.

Amesema ilikua ngumu kuvumilia kuona Man Utd ikipoteza muelekeo, lakini kwake alijua ulikua ni ugeni na utambulishi mpya wa falsafa za meneja huyo kutoka nchini Scotland ambaye kwa sasa yupo nchini Hispania akikinoa kikosi cha Real Sociedad.

Kitabu kilichozinduliwa na mzee huyo kuhusu maisha yake ya ndani na nje ya soka, kinakua cha pili na amejaribu kuzungumzia kila hatua aliyopitia ikiwa ni muendelezo wa toleo la kwanza ambalo alililotoa mara alipotangaza kujiweka pembeni katika tasnia ya ufundishaji wa soka.

‘Magufuli arudishe kadi ya CCM kwa Lowassa’
Rasmi NI Star Times First Division League