Kufuatia taarifa za kuteuliwa kwa klabu ya Singida Utd kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi, imefahamika kuwepo kwa makubaliano kati ya uongozi wa klabu hiyo na kocha mkuu Hans Van der Pluijm.

Katika michuano hiyo Singida Utd imepangwa kuanza kupambana na Mlandege, Desemba 29 katika uwanja wa Amani mjini Unguja saa 8:30 mchana.

Sehemu ya makubaliano kati ya uongozi na kocha huyo kutoka nchini Uholanzi, ni kuhakikisha anatwaa ubingwa wa michuano hiyo ambayo huibua jisisa za ushabiki baina ya klabu za visiwani Zanzibar na Tanzania bara.

Mkurugenzi mtendaji wa Singida Utd Festo Richard Sanga amesema, lengo lao kubwa ni kuona wanafanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo, licha itakua ni mara yao ya kwanza kushiriki.

Singida imepangwa Kundi B ikiwa pamoja na Yanga, Mlandege, Taifa Jangombe, Zimamoto na JKU.

Timu zilizopo Kundi  A ni URA, Jamhuri, Mwenge, Simba na Azam FC.

Mfumo wa usajili watengamaa
Raundi ya pili kombe la shirikisho kuanza kesho