Klabu ya soka ya Simba imemsajili mshambuliaji wa Ndanda FC, Vitalis Mayanga kwa ajili ya kuitumikia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo timu hiyo ipo hatua ya makundi.

Simba imemsajili Mayanga ikiwa ni siku moja tu tangu winga wake, Shiza Kichuya ajiunge na klabu ya Pharco ya Misri ambayo nayo imemtoa kwa mkopo kwenda klabu ya ligi kuu ya Misri Enppi.

Aidha, taarifa ya Simba imethibitisha kuwa nyota huyo tayari amepata leseni ya shirikisho la soka Afrika (CAF) na atatumika kwenye michuano hiyo.

”Mayanga amejiunga rasmi na klabu yetu, sasa yeye pamoja na beki Zana Coulibaly wamepata leseni za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zinazowapa fursa ya kuichezea Simba kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” imeeleza taarifa ya Simba.

Leo, Simba itakuwa dimbani nchini Misri kwenye uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria kukipiga na Al Ahly kwenye mechi ya tatu Kundi D.

Mwanajeshi aliyetoroka jela yenye ulinzi mkali arejea nyumbani
RC Songwe awashukia TBA kuhusu ujenzi wa nyumba za serikali