Klabu ya Simba kwa kushirikiana na Jumia wamezindua huduma ya kununua jezi za Simba 2015 – 2016 kupitia duka la mtandao linalopataikana katika tovuti ya Jumia.

Dhumuni la huduma hii ni kuwapatia wapenzi wa klabu ya Simba njia bora ya kuweza kununua jezi halisi popote walipo Tanzania.

Kupitia mtandao imara na wenye uzoefu wa Jumia, klabu ya Simba inapanga kuongeza upatikanaji wa vifaa vyake ya michezo nchi nzima.

Mkataba huu utaongeza usambazaji wa vifaa vya michezo vya klabu ya Simba.

“Kutokana na kasi ya ukuaji wa upatikanaji wa internet (mtandao), klabu ya Simba inafahamu umuhimu wa kuvifanya vifaa vyake vya michezo kuweza kupatikana kiurahisi kwa wateja wake, hivyo leo tunajivunia kuzindua huduma hii ya Jumia – Simba Online Shop kwa ajili ya kutumia mtandao wa Jumia kuwezesha wapenzi wa Simba popote walipo kuweza kununua mavazi na bidhaa az Simba kiurahisi na kwa bei nafuu”. Alisema Rais wa Simba Evans Aveva

Maneja wa Jumia nchini Tanzania Jean –Philippe Boul aliongeza kwa kusema “uzinduzi wa jezi za mpira wa miguu siku zote ni tukio muhimu kwenye maisha ya klabu maarufu na inayopendwa kama Simba.

Katika msimu wa 2015 – 2016 klabu ya Simba imeamua kuwa wabunifu kwa kutoa fursa kwa wapenzi wake kununua jezi za msimu 2015 – 2016 kupitia njia ya mtandao.

 

“Tunawahamasisha wapenzi wa Simab popote walipo Tanzania kuagiza jezi kupiti tovuti ya jumia.co.tz kuona urahisi katika kufanya manunuzi. Popote walipo wapenzi wa Simba wanaeza kuagiza jezi kupitia touti ya jumia na kuletewa mzigo wako mpka mlangoni. Jumia pia inatoa njia tofauti za ulipia kama ile kuweza kulipia pindi mzigo wakoutakapofika au kufanya malipo kwa njia za kipesa kupitia simu za mkononi. Kuanzia jumatatu 27 – 7 – 2015 wapenzi wa Simba watapatafursa ya kuagiza jezi kupitia tovuti hiyo,” aliongeza Maneja wa Jumia nchini Tanzania Jean –Philippe Boul.

Kuzungumzia mapinduzi haya makubwa katika usambazaji wa vifaa ya michezo ya klabu ya Simba Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya EAGgroup Limited Imani Kajula ambao ni washauri na watekelezaji wa masuala ya kibiashara wa klabu ya Simba alisema “kwa mapinduzi haya makubwa yataiwezesha klabu ya Simba kuongezamapato yake pia kudhibiti bidhaa feki, kupitia Jumia Online Shops (duka la mtandao la Jumia) wapenzi wa Simba watanunua bidhaa za Simba kupitia washirika halali wa uuzaji wa bidhaa za Simba Tanzania.

Dkt. Salim Awaasa Wanasiasa Wanaochungulia Ikulu
Ukawa Wamvua Lowassa Taji La Miba