Kuelekea dirisha dogo la usajili hivi karibuni, inaelezwa kuwa mabosi wa Simba wameanza mchakato wa kunasa saini ya kiungo Anthony Akumu kutoka Zesco ya Zambia.

Kiungo huyo matata ambaye ni raia wa Kenya ameingia katika rada za Simba ili kuboresha zaidi safu ya kiungo ya klabu hiyo.

Taarifa zinasema kuna mabosi wa Simba wanaweza kumnasa kiungo huyo kua kuchukua nafasi ya mchezaji wa kigeni ambaye hadi sasa haijafahamika atakuwa nani.

Aliyekuwa kocha Yanga apata ‘shavu’ Zambia

Simba hadi sasa ina viungo kadhaa ambao baadhi yao ni Jonas Mkude, Clatous Chama, Gerson Fraga na Francis Kahata.

Ikumbukwe leo hii kikosi hiko cha Simba kitashuka dimbani kucheza dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Kijana aliyeishi na vidole 9 kwenye mguu mmoja atimiza nadhiri yake
Kasoro uchaguzi serikali za mitaa zamuibua Mbatia

Comments

comments