Klabu ya Simba imetangaza kupata kocha mpya atakayerithi mikoba ya Kocha Joseph Omog aliyeondoka hivi karibuni kutokana na kushindwa kupata matokeo mazuri.

Kocha huyo mpya wa Simba ni Mfaransa Pierre Lechantre ambaye ametua kuungana na kocha msaidizi Masoud Djuma ambaye alikuwa akikaimu nafasi hiyo baada ya kuondoka kocha Omog.

Lechantre ana uzoefu wa kufundisha soka barani Afrika kwa mafanikio ikiwemo Timu ya Taifa ya Cameroon iliyotwaa ubingwa wa Afrika mwaka 2000 na alishawahi kuwa kocha bora barani Afrika mwaka 2001 huku mwaka 2012 akiwa kocha bora wa Bara la Asia.

Kocha Lechantre ametua nchini na kocha wa viungo raia wa Morocco, Mohammed Aymen Hbibi na jana alipata fursa kushuhudia mchezo wa Simba na Singida United, ambao Simba ilishinda mabao 4-0.

Kiganja: sio kila mgogoro unakwenda BMT
Vigogo wa Six Telecoms wazidi kusota rumande