Klabu ya Simba itawakosa wachezaji wake watatu Haruna Niyonzima, Juma Luzio pamoja na Shomari kapombe katika mchezo wao wa tatu wa Ligi kuu Tanzania Bara Jumapili hii dhidi ya Mwadui FC ya mkoani Shinyanga mchezo utakao chezwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kocha msaidizi wa wekundu wa msimbazi Jackson Mayanja amesema kuwa atawakosa wachezaji wake watatu ambao wote ni majeruhi.

‘’katika mchezo wetu wa jumapili dhidi ya Mwadui ni wachezaji watatu pekee ambao hatuta kuwa nao ambapo Haruna Niyonzima ameumia wiki hii mazoezini, Juma Luzio anasumbuliwa na maralia na Shomari kapombe anasumbuliwa na nyonga pamoja na kifundo cha mguu’’ amesema Mayanja.

Hata hivyo, Kocha huyo msaidizi wa klabu ya Simba amesema kuwa pamoja na kuwakosa wachezaji hao watatu kikosi chake kilichobaki kiko vizuri na wamejipanga kuweza kushinda mchezo huo ili kuzidi kujiwekea mazingira mazuri ya kuelekea katika ubingwa.

Simba SC iliuanza msimu huu wa Ligi Kuu kwa ushindi mnono wa magoli 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting mchezo uliochezwa Agosti 26 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na baadaye  kati amchezo wao wa pili Simba ilipata sare ya 0-0 na wana lamba lamba Azam FC katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Septemba 9.

UN yaziweka mtegoni Tanzania, Uganda kuhusu Korea Kaskazini
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Septemba 15, 2017

Comments

comments