Aliyekuwa mbunge wa bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Shy-Rose Bhanji amelalamikia kitendo cha jina lake kukatwa katika kinyang’anyiro cha kutetea nafasi hiyo katika muhula ujao bila kuhojiwa juu ya tuhuma zilizopelekea jina lake kukatwa.
Pamoja na malalamiko hayo, Shy-Rose Bhanji ametumia fursa hiyo kuwapongeza wanachama waliochaguliwa kuwa wagombea wa bunge la Afrika Mashariki kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi na kuwashukuru wabunge kwa kumpigia kura zilizomuwezesha kuwa miongoni mwa wagombea wanne wa muhula uliopita waliopata kura nyingi zaidi.
“Ingawa jina langu limekatwa na Kamati Kuu ya Chama bila ya mimi nwenyewe kuitwa na kuhojiwa ili nipewe haki ya kujibu hoja zozote dhidi yangu, nawapongeza wote waliochaguliwa kuwa wagombea wa EALA kupitia CCM. ninawashukuru sana wabunge kwa kunipigia kura nyingi zilizoniwezesha kuwa miongoni mwa wagombea wanne wa mwanzo walioongoza kwa kura,” amesema Shy-Rose Bhanji.
Hata hivyo, amefikia hatua hiyo baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kutangaza majina 12 ya wanachama wake watakao chuana ili kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki huku jina lake likiwa limeenguliwa.

Magazeti ya Tanzania leo Machi 31, 2017
Video: DC Mjema azindua kampeni ya upandaji miti