Mbunge wa Singida Mashariki, na Rais wa Mawakili Tanganyika (TLS), Tundu Antipas Lissu, ameshindwa kugombea nafasi ya Urais wa cha hiko cha Mawakili kwa awamu ya pili kutokana na kutokukidhi sheria mpya zilizoundwa kwa wagombea wa nafasi hiyo.

Ambapo Lissu kwa mara nyingine aliteuliwa kugombea nafasi hiyo mara baada ya kuwasilisha barua yake ya uteuzi kwenye sekretarieti hiyo na kushindwa kukidhi matakwa mapya yaliyotolewa.

Kufuatia kanuni mpya iliyopendekezwa kwa mgombea wa Urais TLS, kifungu cha nne kinamzuia mtu ambaye ni kiongozi wa chama chochote cha siasa kuongoza chama hicho.

Kanuni hiyo inamfunga moja kwa moja, Tundu Lissu ambaye anaitumikia Serikali kwa kuwaongoza wamanchi wa Singida Mashariki, hivyo kwa mujibu wa sheria hiyo Lissu hawezi kugombea nafasi hiyo tena mpaka pale watakapofanya marekebisho ya sheria hiyo.

Aidha Lissu ameweza kutumikia nafasi hiyo kama Rais wa TLS, kwa muda wa miezi sita mpaka pale aliposhambuliwa na Risasi mnamo Septemba 7 mwaka jana, amekaa hospitalini kwa matibabu kwa muda wa miezi sita , kwa sasa yupo nchini Ubelgiji akiendelea na matibabu ya majeraha aliyoyapata pindi aliposhambuliwa na risasi Dodoma.

 

Meek Mill amkataa tena Jaji
Fatma Karume kumg’oa urais Lissu