Serikali ya Uganda kupitia Wizara ya Utamaduni na Sanaa imetangaza sheria mpya zenye lengo la kuwabana wasanii, ili kulinda maadili na sanaa kwa ujumla.

Sheria hizo ambazo zimetangazwa wiki iliyopita, zinaeleza kuwa msanii yeyote hawezi kwenda nje ya nchi kutumbuiza bila kibali .

Sheria nyingine ni kwamba msanii yeyote wa muziki hatakiwi kupanda jukwaani akiwa amevaa nguo fupi au mlegezo.

Sheria nyingine, msanii hataruhusiwa kupanda jukwaani kutumbuiza akiwa ametumia kinywaji au kilevi cha aina yeyote.

Mabadiliko hayo pia, yanamtaka kila msanii asajiliwe na haitaruhusiwa wimbo uachiwe bila kukaguliwa na mamlaka husika ya serikali.

Lakini pia sheria inzamtaka msanii kuzingatia kanuni za usafi kabla ya kupanda kwenye stage kufanya shoo.

 

Hata hivyo, mabadiliko hayo yamepelekea baadhi ya wasanii akiwemo Eddy Kenzo kuandaa mikutano ya kushinikiza sheria hizo zilegezwe.

Jaribio lingine la Al-Shabaab lazimwa Kenya, wakimbizwa
Wazazi wawalazimisha watoto wajaze madudu mtihani darasa la saba