Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein ametaja sababu za kutokuwepo kwa baadhi ya viongozi kwenye maadhimisho ya miaka 55 ya mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumza kwenye hadhara hiyo hapo jana Rais Shein alisema kuwa sababu iliyowafanya Rais mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, pamoja na Rais wa sasa Dkt. John Pombe Magufuli kuwa ni viongozi kupatwa na dharula.

Aidha, Rais Shein amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake itaendelea kulinda usalama wa nchi na kudumisha upendo, amani na mshkamano kwa wote

“Ninawahakikishia kuwa nchi yetu iko salama na itaendelea kubaki salama na serikali zetu mbili zitaendelea kutimiza majuku yake ipasavyo na tutahakikisha amani na utulivu vinadumishwa na sheria zote zinafuatwa.”alisema Dkt. Shein

Hata hivyo, ameongeza kuwa yeye na rais Magufuli watahakikisha Muungano unadumu kwa dhamira ile ile ya viongozi waliopita ili nchi izidi kubaki na amani.

Makumi wapoteza maisha kwenye mlipuko wa tenki la mafuta
Mo Dewji awapa nguvu zaidi Simba