Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein, ametoa msamaha kwa wafungwa 12 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais Shein ametoa msahama kwa wafungwa hao ambao walikuwa wamehukumiwa kwa makosa mbalimbali.

Msamaha huo umetolewa kwa mujibu wa ibara ya 59 ya Katiba ya Zanzibari ya mwaka 1984 ambayo imempa Rais mamlaka ya kutoa msamaha kwa wafungwa.

Msamaha huo unatolewa kwa wafungwa kama nafasi ya wao kuanza kuishi maisha mapya na kuachana na vitendo vya kihalifu.

Majina ya wafungwa waliopewa msamaha ni, Abdul-Aziz Abdalla, Omar Abdalla Nuhu, Ali Khamis Mrau, Mussa Ali Vuai, Hassan Seif Khamis,  Nassor Abeid Issa, Jihadi Jalala Jihadi,  Edward Jemeria Magaja, Sleiman Abdalla Amir, Mtumwa Khamis,  Said Seif Omar,  Masoud Seif Nassor.

 

 

Tukumbushane tafsiri 4 za kumpa mwenza wako zawadi
Video: Watanzania waombwa kuendelea kumchangia matibabu mtoto aliyefanyiwa operesheni 10 bila nafuu