Meneja wa klabu ya Leicester City, Craig Shakespeare amesema kiungo wake Riyad Mahrez yupo tayari kuanza mchezo wa leo Ijumaa.

Leo ndiyo siku ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya England ‘Premier League’ kwa mchezo mkali kati ya Arsenal dhidi ya Leicester City kwenye Uwanja wa Emirates.

Awali, Arsenal walikuwa wakimtaka kiungo huyo raia wa Algeria na Leicester wakatangaza kuwa hawawezi kumuuza, lakini mwanzoni mwa msimu huu walimtaka tena ingawa anawaniwa kwa nguvu kubwa na AS Roma ambao walipeleka ofa ya pauni milioni 32, ikakataliwa.

Maximo Amfanyia Kampeni Mwakalebela

“Sina jambo lolote ambalo linaweza kunizuia kumuanzisha, naweza tu kuzungumza jinsi timu yangu itakavyocheza, lakini hakuna hofu ya kumchezesha.

“Najua kuwa Arsenal walikuwa wanamtaka lakini hapa yupo kazini na naamini kuwa ataonyesha kiwango cha juu kwa kuwa yupo vizuri kiakili.

“Hatujagoma kumuuza, lakini tunahitaji anunuliwe kwa thamani yake halisi, na ikishindikana basi atabaki hapa,” alisema meneja huyo.

Huu utakuwa mchezo wa kwanza mkubwa kwa Arsenal baada ya mwishoni mwa juma lililopita kucheza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Chelsea na kushinda kwa penati 4-1, baada ya sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90

Zlatan Ibrahimovic Kurudishwa Old Trafford?
Maximo Amfanyia Kampeni Mwakalebela