Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Isack Kamwelwe ameshuhudia hafla ya utiaji saini baina ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na kampuni nne za simu za mkononi ambazo zimepatiwa ruzuku na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya shilingi bilioni 173 ya kupeleka huduma za mawasiliano vijijini kwenye kata 173 za zilizopo kwenye maeneo mbali mbali nchi nzima. Kampuni nne zilizosaini mkataba na UCSAF ya kupeleka mawasiliano ni Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Kampuni ya Vodacom Tanzania, Kampuni ya Viettel Tanzania (Halotel) na Kampuni ya MIC Tanzania (TIGO).

Amesema kuwa dunia hivi sasa iko kiganjani ambapo kila mwananchi anatakiwa apate mawasiliano ya uhakika kama ambavyo Ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyotutaka kuhakikisha serikai inawapatia Watanzania wote huduma za mawasiliano

“Tumekubaliana na Shirika la Posta Tanzania (TPC) kuwa waanze kutoa huduma za kifedha na watumie huduma za Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ili mawasiliano yaweze kufika vijijini kwa kuwa TPC na TTCL ni taasisi kongwe na wana mtandao mpana wa ofisi zao nchi nzima”, amesema Kamwelwe.

Aidha, amesema kuwa kampuni za simu za mkononi zililenga zaidi kutoa huduma za mawasiliano mijini ila Serikali ikaone ni muhimu ianzishe Mfuko wa UCSAF ili ipeleke mawasiliano kwa wananchi wote vijijini na kwenye maeneo ambayo hayana mvuto wa kibiashara.

Kwa uande wake, Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Mhandisi Peter Ulanga amesema kuwa kampuni nne za mawasiliano za simu za mkononi zimeshinda zabuni ya Awamu ya Tatu ya kupeleka mawasiliano kwenye kata 178 kwa gharama ya shilingi bilioni 28, na kuongeza kuwa hadi hivi sasa UCSAF imepeleka mawasiliano kwenye jumla ya kata 703 nchi nzima kwa kujumuisha awamu za awali za mradi.

 

Mahakama yamshushia rungu Rais wa zamani, ‘alipe’
Nicki Minaj aapa kumburuza mtangazaji huyu mahakamani