Naibu Waziri wa Wizara ya Madini, Stanslaus Nyongo amewaeleza wahasibu wa madini nchini kuwa wizara haitamvumilia mtu yeyote ambaye atakuwa chanzo cha upotevu wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
 
Ameyasema hayo wakati akifunga Mafunzo ya Kielektroniki ya Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali ambayo yaliaanza tarehe 12 hadi 15 Novemba, 2018 katika Chuo cha Mazimbu Campus kilichopo mkoani Morogoro.
 
Amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuongeza tija na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato serikalini. ambapo amesema kuwa Viongozi wote wako tayari kutoa msaada wowote masaa 24 hivyo kama kuna mhasibu ambaye atakuwa na uhitaji kwa masuala ya kikazi asisite kuwasiliana nao waati wowote.
 
Aidha, amesema kuwa tasnia ya uhasibu ni ya muhimu sana katika sekta ya madini, hivyo ni vyema kila mmoja wao kuhakikisha kuwa katika malengo yake akahakikisha kuwa anafikia lengo la ndani la Wizara la ukusanyaji wa Bilioni 500 linatimizwa.
 
  • Diwani wa Chadema afikishwa Mahakamani
  • Magunia 17 ya Bangi yakamatwa mkoani Pwani
  • Meya wa Iringa adaiwa kukamatwa akipokea rushwa
 
Hata hivyo, Nyongo amemtaka Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Shukurani Manya kuhakikisha kuwa kunakuwa na utekelezaji wa maazimio yote waliyoyafikia katika mkutano huo ili kuweza kuboresha utendaji wao na kuongeza mapato ya wizara kwa mwaka wa fedha 2018/19.

Vijana ambao hawajaoa kuanza kulipa kodi
Video: Makonda afanya ziara mkoani Morogoro