Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amesema wamevunja mkataba wa zaidi ya Trilioni 1 kati ya Jeshi la Zimamoto na Kampuni ya ROM Solutions ikiwa ni agizo la Rais dkt. John Magufuli aliyesema mkataba huo una mapungufu mengi.

Simbachawene amesema mkataba huo kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya Jeshi la Zimamoto umevunjwa kwakuwa hauna tija kwa Taifa, na hakutakuwa na hasara au madai yoyote kutokana na pande zote kuridhia kuvunjwa kwake.

Aidha amebainisha kuwa aliyekuwa kamishna jenerali wa jeshi la zimamoto, Thobias Andengenye hakuwa na sifa za kufanya mkataba huo.

“kutokana na ukubwa wa mkataba na kiwango cha fedha, kamishna hakuwa na sifa za kusaini kwakuwa aliyetakiwa kufanya hivyo ni waziri wa fedha” amesema Simbachawene

Mkataba huo ulipelekea aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola na aliyekuwa Kamishna wa Jeshi hilo, Thobias Andengenye kuondolewa katika nafasi zao.

Halima Mdee, Ester Bulaya warudishwa selo
Jamhuri yapinga maombi ya Rugemalira kuachiwa na Mahakama

Comments

comments