Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) imesema kuwa imetenga kiasi cha Sh. milioni 700 kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kufuga nyuki kwa njia ya kisasa kwa mikoa nane.

Hayo yamesemwa mkoani Geita na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constanine Kanyasu wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Ametaja baadhi ya wilaya katika mkoa wa Geita zitakazonufaika na mradi huo kuwa ni wilaya ya Ushirombo pamoja na Mbogwe.

Amezitaka wilaya hizo kujiepusha na ukataji miti ovyo kwa vile nyuki ni rafiki wa mazingira badala yake zijikite zaidi  katika kupanda miti.

Aidha, Kanyasu amesema kuwa wafugaji hao wataokuwa wamejiunga katika vikundi hivyo watapatiwa elimu ya ufugaji nyuki kwa njia ya kisasa pamoja na kuwezeshwa pesa zitakazotumika kwa ajili ya kununulia mizinga ya kisasa itakayosaidia kuzalisha mazao ya nyuki yatakayokidhi soko la kimataifa.

Hata hivyo, kufuatia hali hiyo amesema Wizara imedhamiria kuleta mapinduzi katika uzalishaji wa mazao ya nyuki kwa kuwawezesha wananchi kufuga kisasa hali itakayosaidia wananchi kuwa mstari wa mbele katika kulinda na kuhifadhi misitu

Wafuasi wa Chadema watimuliwa mahakamani
Video: Hoja saba kuwatoa Mbowe, Matiko leo? Rushwa ya ngono UDSM yachukua sura mpya

Comments

comments