Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa kesho Aprili 26, 2019 ni siku ya mapumziko na hakutakuwa na shamrashamra za sherehe.

Waziri Mkuu hayo ofisini kwake jijini Dodoma leo Aprili 25, 2019, ambapo ameeleza kuwa kesho ni siku ya mapumziko kitaifa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lakini hakutakuwa na sherehe.

Amesema jumla ya shilingi milioni 988.9 ambazo zilikuwa zimepangwa kwa ajili ya sherehe hizo, zimeokolewa na zitapangiwa shughuli nyingine.

Video: Spika amshukia Zitto sakata la CAG, Kimbunga Kenneth kutikisa
Video: Sugu ajitokeza kumpokea Magufuli Mbeya