Serikali imetangaza kusitisha zoezi la kutoa maeneo mapya ya utawala hadi pale itakapotangaza kuanza kwa mgawo huo ambapo itatangaza kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa katika mikutano ya hadhara iliyofanyika Ulyankuru na Kaliua Wilayani Kaliua mkoani Tabora.

Akizungumzia kuhusu migogoro baina ya wanavijiji na maeneo ya hifadhi, Majaliwa amesema kuwa Serikali bado inafanya uhakiki wa mipaka katika maeneo ya hifadhi na ikikamilisha zoezi hilo itatoa taarifa.

“Kwa sasa tumesitisha kutoa maeneo mapya ya utawala ili tuimarishe kwanza yale ya awali. Tunaimarisha kwanza miundombinu ya majengo ya ofisi,  nyumba za watumishi kwenye wilaya na Halmashauri mpya, zikitengamaa tutafanya maamuzi mapya, ” amesema Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka wananchi wanaoishi pembezoni mwa vijiji vinavyopakana na maeneo ya hifadhi, wasifanye upanuzi wowote hadi zoezi la kuhakiki mipaka ya hifadhi litakapokamilika.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali inafanya mapitio na ikilazimu itabidi ifanye marekebisho ya Sheria inayohusu Misitu ya Hifadhi pamoja na Sheria inayohusu masula ya Wakimbizi

China yamuonya Trump kuhusu matamshi
Majina ya watuhumiwa sugu wa uporaji yaanikwa

Comments

comments