Serikali imatoa ajira kwa watumishi 2,160 katika shule za sekondari nchini ambapo kati yao waalimu 1900 ni wa masomo ya sayansi na hisabati.

Akizungumza, Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amesema kati ya watumishi hao walioajiriwa 100 ni waalimu wa lugha na 160 ni fundi sanifu maabara.

Amesema watumishi hao wanatakiwa kuripoti katika ofisi za wakurugenzi wa halmashauri zilipo shule walizopangiwa kuanzia Agosti 23, 2018 hadi Septemba 5, 2018.

Watumishi hao wanatakiwa kuripoti kwa muda huo wakiwa na vyeti vya taaluma vya kidato cha nne na kidato cha sita, vyenye halisi vya kitaalam vya mafunzo ya ualimu vya ngazi husika pamoja na cheti cha kuzaliwa, na hatimaye kwenye shule walizopangiwa” amesema Jafo.

Hata hivyo, Jafo amewataka waajiriwa hao kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi na si makao makuu ya halmashauri ili kuomba kuhamishiwa vituo vya kazi.

”Mwajiri yeyote atakayechukua posho ya kujikimu kisha asiripoti kwenye kituo chake cha kazi serikali itamchukulia hatua za kinidhamu” aliongezea Jafo.

Jafo ametumia nafasi hiyo kuwataka wakurugenzi wa halmashauri zenye vituo vya kazi walizopangiwa watumishi hao kuwapokea na kwa kufuata taratibu zote na kanuni za utumishi.

DC Mjema aunda mkakati wa kudhibiti uhalifu Ilala
Mnangagwa amtumbua aliyempa mke wa Mugabe PhD