Serikali kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekanusha taarifa za kuwepo kwa mlipuko wa Ugonjwa wenye dalili zinazofananishwa na za Malaria katika jiji la Dar

Kanusho hilo linakuja kufuatia kuwepo kwa taarifa kwenye Mitandao mbalimbali ya Kijamii kuhusiana na uwepo wa hali ya homa kali, inayoambatana na kukohoa, mafua na maumivu makali ya kichwa kwa baadhi ya watu katika maeneo ya mkoa wa Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Dkt. Faustine Ndugulile amesema, wizara imeziona taarifa hizo na inaendelea kufuatilia kupitia timu ya wataalamu wa uchunguzi kwa kushirikiana na timu ya mkoa wa Dar es salaam

“Timu yetu inaendelea kufanya mahojiano ya kitaalamu na wanaodaiwa kuugua ugonjwa huo na pia kupitia taarifa za wagonjwa wenye dalili kama hizo katika vituo vya kutolea huduma ili kuzichambua na kuzitolea ufafanuzi” alisema Ndungulile.

Hata hivyo Dkt Ndungulile amewataka wamiliki wa vituo binafsi na vituo vya umma kuzingatia miongozo yote ya matibabu na ile ya utoaji wa taarifa endapo wanahisi kuna ongezeko la ugonjwa wa aina yoyote kuliko kawaida.

Ambapo amesema jamii inapaswa kuzingatia kanununi za afya na usafi wa mazingira ili kujikinga na magonjwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha inafanya usafi binafsi.

Aidha aliwataka wananchi kuwa watulivu na kuwa na imani na matibabu katika vituo vya kutolea huduma amabvyo vimeimarishwa kwa kasi kubwa katika serikali ya awamu ya tano.

Wakati huohuo, Serikali imekiri kuwepo kwa mlipuko wa Ugonjwa kuharisha katika Jiji la Dodoma huku ikitoa tahadhari kwa Wananchi kuendelea kuchukua hatua za kujikinga ikiwemo kuzingatia suala la usafi

Mvua ya simamisha shughuli Dar es Salaam, Mbowe atoa onyo kali
Boeing kutozalisha ndege za 737 Max kuanzia Januari 2020