Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefuta mitihani ya kidato cha pili visiwani humo iliyokuwa ikiendelea na kusema kuwa tarehe ya mitihani hiyo itatangazwa tena.

Akizungumza na wanahabari Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Riziki Pembe amesema kuwa mitihani hiyo ifutwe na wanafunzi waendelee na masomo yao kama kawaida.

“Wizara imefuta mitihani hiyo na itatangaza tena tarehe ya kurudiwa, mara tu taratibu zitakapo kamilika”amesema Pembe

Hata hivyo, mitihani hiyo imeahirishwa ikiwa ni muda mfupi tangu kwa upande wa Tanzania bara, kukamilisha mitihani hiyo Novemba 24.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 4, 2018
Manaibu waziri wasisitiza usimamizi mzuri wa Wakandarasi