Serikali nchini Angola imefunga makanisa 34 kufuatia oparesheni maalum iliyopewa jina la Operação Resgate (Oparesheni Okoa).

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Idara ya Polisi ya Taifa, Orlando Bernardo amesema kuwa oparesheni hiyo maalum inayofanywa na polisi imefunga makanisa 19 katika jimbo la Cabinda, 11 katika eneo la Luanda na manne katika jimbo la Malanje.

Akieleza sababu za kuyafungia makanisa hayo, Bernardo  alisema kwa mujibu wa taarifa waliyonayo, makanisa 1,116 nchini humo yanaendesha shughuli zake kinyume cha sheria na kwamba makanisa hayo yote lazima yachukuliwe hatua pia.

Serikali imeeleza kuwa zaidi ya nusu ya makanisa nchini humo yanaendeshwa na raia wa kigeni, wengi wakitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Brazil, Nigeria na Senegal.

‘Oparesheni Okoa’ iliyoanza Novemba 6 mwaka huu inatarajia kudumu hadi mwishoni mwa mwaka huu.

Meya wa Iringa adaiwa kukamatwa akipokea rushwa
Polisi wahukumiwa kifo kwa kumuua mlinzi wa Mbunge