Mpango wa lipa kulingana na matokeo EP4R umechangia kupunguza ndoa za utotoni kwa wanafunzi wanaokaa mbali na shule kwa wilaya ya Ruanga mkoa wa Lindi.

Akiongea na timu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari na maafisa wa Elimu mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Ruanga, Herbert Ngonuani amesema kwa kipindi cha nyuma walipokea kesi za wanafunzi 994 wa kike, watano kupata mimba hali iliyopelekea kukatisha masomo yao wakiwa wadogo na kuongeza idadi ya watu wasio na elimu ya kusoma na kuandika.

Amesema mradi huo wa EP4R umesaidia kuboresha na kujenga majengo ya vyumba vya madarasa, mambweni, bwalo lakulia chakula pamoja na vyoo vya wanafunzi wenye ulemavu kuhudhuria masomo yao kila siku na kufwata maadili wanayofundisha na walimu wao.

Serikali kupitia wizara ya elimu, sayansi, teknolojia ilipeleka zaidi ya shilingi Milioni 200 katika shule ya sekondari Ruanga kwa ajili ya Bilioni 2.8 zilizotolewa kwaajili ya zoezi hilo kwa mkoa wa Lindi.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Mpina acharuka kuhusu vibudu vilivyokamatwa Jijini Dar
Rais John Magufuli akubali kuwakabidhi kombe Simba SC