Serikali imeagiza kusajiliwa kwa mafundi wanaotengeneza simu nchini ili mafundi hao waweze kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria, na kutoa huduma zenye viwango na ubora.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Dkt, Jim Yonaz alipokuwa akiwatunuku vyeti vya mafunzo ya miezi 5 mafundi simu 68, ambayo yalitolewa na Chuo cha Sayanasi na Teknolojia DIT.

Amesema kuwa hatua ya TCRA kuwatambua mafundi hao ni muendelezo wa kuunga mkono juhudi za kuelekea uchumi wa viwanda ambayo ni sera ya serikali ya awamu ya tano.

“Kuanzisha mafunzo haya ya kurasimisha ufundi wa simu za mkononi kutawasaidia mafundi kufanya kazi kwa weledi na ufahamu lakini pia itaisaidia TCRA kutoa leseni kwa mafundi ambao kiwango chao kinafahamika,”amesema Dkt. Yonaz

Hata hivyo, Mwaka 2016 serikali kupitia mamlaka ya Mawasiliano Tanzania  TCRA iliendesha zoezi la kuzifungia simu feki ambazo zimeingia nchini bila ya kuwa na imei namba ambapo kupitia zoezi hilo maelfu ya wamiliki wa simu na wafanyabiashara wa simu walipoteza simu zao.

 

Mahakama yamfungulia Mdee mipaka
Wafanyakazi wacharukia kanuni mpya za mafao, ‘haiwezekani’