Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa miongoni mwa mambo yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano ni Serikali kuwa na msimamo thabiti kwenye baadhi ya miradi ambayo imeamua kuitekeleza.

Amesema kuwa Serikali ya awamu ya 5 imekuwa na msimamo mkali kwenye miradi yake, toka imeanza kwenye bajeti ya kwanza mpaka bajeti ya nne.

“Kuna mradi wa reli, hela za ununuzi wa ndege kwenye bajeti ya pili na tatu fedha zimeongezeka, ukiendelea mtiririko kwenye bajeti ya kwanza mpaka ya nne tunayoijadili, utaona kwamba Serikali imetatua tatizo la kutokuwa na msimamo kwa hiyo hii ni chanya kwa Serikali.” amesema Zitto

Aidha, amesema kuwa changamoto kubwa iliyopo katika miradi iliyoamuliwa kutekelezwa na Serikali, miradi hiyo fedha zinaenda nje na haingizi fedha kwenye uchumi na matokeo yake mzunguko wa fedha ni mdogo, na ndiyo maana ukuaji wa uchumi umekuwa ni mdogo.

Hata hivyo, ameongeza kuwa pamoja na wapinzani kuikosoa serikali lakini imekuwa ikifanya mambo makubwa na mazuri kwa kufanya kile wanachokiamini na kukisimamia na hatimaye kutoa mafanikio mazuri.

TRA yatangaza adhabu kali kwa wasiodai wala kutoa risiti
Video: Mambo 6 usiyofahamu kuhusu Simba 'Mfalme wa nyika'