Gavana wa Benki Kuu ya Kenya (CBK), Patrick Njoroge ametangaza kuwa Serikali itaweka karantini pesa zote kutoka benki kwa kipindi cha wiki moja.

Hatua hiyo ni mikakati ya serikali kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa COVID-19 ambao pia unasambazwa kupitia pesa.

Njoroge aliwahimiza Wakenya kufanya miamala kwa njia ya simu ili kutekeleza shughuli zao kama hatua ya kupunguza kusambaa kwa virusi hivyo.

Mkuu huyo wa CBK pia alitangaza kuwa itakuwa afueni kwa wanaokopa mikopo kulindwa dhidi ya athari za coronavirus kwa uchumi. “Kudhibiti athari za COVID-19 katika jamii, benki zitapata afueni ya kutoa mikopo,” alisema Njoroge.

Kulingana na Njoroge benki zitarefusha kipindi cha kulipa mkopo kwa mwaka mmoja. Aliwashauri wanaokopa kutembelea benki zao kujadiliana mpango wa kulipa mikopo. “Benki zitarefusha muda wa kulipa mkopo kwa mwaka mmoja. Kwa hivyo kama una deni na wapatikana na shida ya kuilipa kwa sababu ya janga la virusi vya corona waeza kutembelea benki yako kujadiliana,” alisema Njoroge.

CORONA: Ligi Tanzania kuchezwa bila mashabiki
Rukwa: wahukumiwa kwa kuoa wahamiaji haramu