Serikali ya awamu ya tano inatarajia kushusha faini ya shilingi 30,000 inayotozwa kwa madereva wa pikipiki kwa kosa moja sawa na faini inayotozwa kwa madereva wa mabasi makubwa (daladala) ikidai kuwa ni faini kubwa  kulinganisha na kipato wanachoingiza katika biashara hiyo.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ambaye amesema tayari swala hilo limekwishawekwa kwenye mapendekezo ya faini Wizara ya Fedha na Mipango na kuingizwa kwenye sheria ya fedha ya mwaka 2018.

Hata hivyo wamegundua kwamba kutokana na kipato wanachokipata kulinganisha na faini hiyo pikipiki nyingi zimejazana katika vituo vya polisi wakishindwa kulipa faini hiyo, hivyo Mwigulu amesema kwa kushusha faini itawasaidia waweze kumudu gharama za faini ambazo wanatozwa.

Aidha Mwigulu amesema kuanzia jana ameanza kutembelea vituo vya polisi kukagua kama agizo lake la kutoshikilia bodaboda vituoni pindi zinapofanya makosa limetekelezwa badala yake ziandikiwe makosa zikafanye kazi ili zipate fedha za kulipa faini hizo.

Hoja hiyo iliibuliwa Bungeni na Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga alipokuwa akiuliza swali la nyongeza na kuhoji ni lini sheria itabadilishwa ili faini za bodaboda wanazobeba abiria mmoja wanapopofanya makosa barabarani ziwe ndogo kuliko mabasi yanayobeba abiria wengi na wote wanatozwa sh. 30,000 kwa kosa moja.

 

Pochettino kubaki Spurs mpaka 2023
Mane akumbuka kijijini kwao akijiandaa kuiua Madrid