Serikali imesema ipo haja ya kurasimisha shughuli zinazofanywa na watu za kuokota chupa na makopo ya maji ili iwe ajira rasmi kwasababu kazi hiyo inasaidia kupunguza uchafu wa mazingira.

Hayo yamesemwa na Waziri wa nchi, ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na mazingira, January Makamba katika mkutano wa kimataifa wa mtandao wa wasakataji na usimamizi wa mazingira ulioandaliwa na Chuo kikuu cha Dar es salaam, shule kuu ya Biashara (UDBS), na wadau mbalimbali wa mazingira wenye lengo la kuzungumzia ukusanyaji wa taka na uchakataji wa taka.

Waziri Makamba amesema kuwa kwasasa majiji mbalimbali nchini yameelemewa na takataka, hivyo kitendo wanachofanya baadhi ya watu cha kuokota chupa za maji kwaajili ya kwenda kuziuza wanafanya kazi nzuri ya kusaidia kupunguza tatizo la uwepo wa taka.

“Kitendo cha watu kuokota makopo ni njia moja wapo ya kufanya mazingira kuwa safi na salama kwani chupa hizo zimekuwa zikisababisha uchafu katika majiji”

Nakuongeza kuwa watu wanaofanya kazi hizo wakati mwingine wanaonekana watu wenye ugonjwa wa akili kutokana na kupita kwenye maduka au majumbani kwa watu, lakini kazi wanayoifanya ni ya kuongeza kipato hivyo Serikali inaona umuhimu wa kuirasimisha kazi hiyo kuwa rasmi.

Hata hivyo Waziri Makamba amesema wakati umefika sasa kwa taasisi za serikali na vyuo kuongeza tafiti zitakazoweza kuleta fursa za kuzifanya takataka kuwa sehemu ya kuongeza kipato kwa taka hizo.

Mratibu Msaidizi wa mkutano huo kutoka UDBS, Dk. Nelly Malima, amesema kuwa katika mkutano huo wamejadili jinsi ya kuweza kuondokana na taka na kuzichakata na kuwa na fursa ya kuongeza kipato.

 

 

 

Video: TUCTA watoa ombi kwa Serikali, JPM awajibu
Wanajeshi 30 wa Nigeria watoweka