Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla amesema kuwa Serikali itaanza kuuza asilimia 10 ya Mamba nje ya nchi kwa kile alichokieleza kumekuwa na ongezeko kubwa sana la Wanyama wakali kuingia kwenye makazi ya watu.

Amesema kuwa Serikali imejitahidi vya kutosha kuhakikisha suala la ujangiri linaisha nchini na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa bali changamoto iliyopo ni Wanyama hao kuingia kwenye makazi ya watu.

Uhifadhi na ulinzi wa maliasili nchini umeimarika na tumepata mafanikio makubwa sana, Ujangili tumeudhibiti kwa mafanikio makubwa sana, Changamoto mpya imezaliwa, wanyama wakali na waharibifu wamezidi na wanavamia maeneo ya watu, tumeamua kuuza asilimia 10 ya mamba wote nchini,”amesema Dkt. Kigwangallah

Aidha, waziri Kigwangallah amesema kuwa Serikali itauza viboko wote waliopo kwenye maeneo yenye maji kama maziwa, mabwawa na mito iliyopo mjini, kama vile Mpanda, Mafia na Babati, mauzo ya wanyama ambayo yatafanyika kwa njia ya mnada kwa utaratibu ambao utatangazwa wiki ijayo.

Pia, waziri Kigwangallah ameongeza kuwa serikali itaanzisha mradi wa kuweka uzio kwenye maeneo yenye historia ya matukio ya Mamba kudhuru watu, kama Maleza na Ruvu, hivyo kuwaomba  wananchi wasifanye tabia hatarishi.

LIVE DAR ES SALAAM: Ufungaji wa mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi za Kusini mwa Afrika SADC
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Agosti 18, 2019