Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Muungano, January Makamba leo Bungeni Dodoma katika mkutano wa 15 kikao cha 5 kwenye kipindi cha maswali na majibu alihojiwa juu ya mkakati wa serikali kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya Plastiki.

Akijibu swali hilo, Waziri Makamba amesema kuwa hadi ifikapo Juni 1, serikali tayari itasitisha matumizi ya mifuko hiyo na kuja na njia mbadala ya kutatua changamoto ya matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo imekuwa chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira hapa nchini.

”Ni kweli kabisa tumeongea na wadau wote na wamesema kuwa hakuna sababu yeyote ya kutumia mifuko ya plastiki hapa nchini mimi kama Waziri wa mazingira nakubaliana na hilo na mbadala upo na unawezekana lakini lazima tukubaliane kwamba tunapopiga marufuku basi tuwe tumejianda kufanikiwa sababu zipo nchi ambazo zimeamua kuchukua hatua hii lakini hazikujiandaa kwenye kufanya hili zoezi, wakajikuta kwamba mnatoa tangazo tuu lakini kitaasisi hamjajipanga kiuratibu hamjajipanga kwahiyo inakuwa ni bure”amesema Makamba.

Aidha, Makamba amesema anataka suala hilo lifanikiwe kwa asilimia kubwa kwani linatarajiwa kutoa ajira kwa watu wengi zaidi.

Video: Watakao andamana Dodoma watapigwa watachakaa - RPC Muroto
Video: Mke wangu nampiga kwa tishu - Foby

Comments

comments