Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Dkt.  Faustine Ndugulile amefungua kongamano la Kisayansi la Hospitali ya Taifa Muhimbili na kusisitiza kuwa serikali imedhamiria kutoa muongozo mpya wa matumizi  ya dawa ili kudhibiti matumizi holela ya dawa.

Amesema kuwa muongozo huo utasaidia kupunguza matumizi holela ya dawa ambayo yanachangia usugu wa dawa katika mwili wa binadamu.

“Muongozo huu mpya utakapotolewa utatumika  katika Hospitali zote nchini na pia serikali tayari imeoredhesha dawa muhimu na dawa hizi zinapatika kwani serikali imeongeza bajeti ya dawa kutoka Shiling bilioni 30 hadi kufikia bilioni 269,” amesesisitiza Dkt. Ndugulile.

Aidha, Dkt. Ndugulile ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa jitihada zake za kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha inapunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Hata hivyo, Muhimbili tayari imeanza kutoa huduma ya kupandikiza figo, kufanya upasuaji wa kuwawekea vifaa vya kuwasaidia watoto kusikia na sasa wataalam wengine wanajiandaa kwenda India ili kujengewa uwezo wa kufanya upasuaji wa kupandikiza Ini.

Kilimanjaro stars yaongeza watatu, kulifuata kombe la Chalenji kesho
Sirro aagiza msako watoto 1,300 kibiti