Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kwa ushirikiana na Wizara ya Mambo ya ndani, na Ofisi ya Rais TAMISEMI imesema itahikikisha Wanawake wote wanaojihusisha na biashara ya ukahaba wanaendelea kukamatwa ili kulinda hadhi ya mwanamke

Hayo yamesemwa Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii, jinsia Wazee na watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla na kuwataka kuacha mara moja na kutafuta shughuli nyingine ya kujiingizia kipato

Aidha, Dkt. Kingwangala ametumia furasa hiyo kuwaasa wanaume ambao ndio wateja wakubwa wa biashara hiyo kuacha mara moja kwani kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria, hivyo yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua kali mara moja.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Serikali imepiga hatua ya kupambana na watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na hatua kadhaa wamezichukua ikiwemo kuzifungia baadhi ya taasisi zilizokuwa zinaashiria kuwasaidia watu wa aina hiyo.

Dunia kushuhudia pambano la mwaka la masumbwi leo, Canelo Vs Triple G
Auawa kikatili kisha ubongo wake kuchukuliwa