Mwanafunzi mmoja wa darasa la nne amepoteza maisha baada ya kukanyagwa na tembo katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Imeelezwa kuwa mwanafunzi huyo alikuwa na mwanafunzi mwenzake ambao wanasoma katika shule ya msingi Guta, wamekanyagwa na Tembo wakati wakivuka kwenye hifadhi hiyo.

Mwenzake wa darasa la kwanza, yeye amejeruhiwa vibaya, huku chombo cha habari Channel Ten kikiripoti kuwa hali hiyo imezua hofu kwa jamii hususani kwa wanafunzi.

Aidha kila siku wanafunzi hutembea umbali wa kilometa 36 kutoka katika kijiji cha Nyatwari kwenda shule ya Kuzungu wilayani Bunda mkoani Mara.

Walimu walioanzisha twisheni kutiwa mbaroni
Tibaijuka ataka tiba mbadala kuingilia kati corona

Comments

comments