Jumla ya nchi saba zitashiriki katika fainali ya kutafuta mwakilishi wa  nchi za Afrika Mashariki na Kati kwa ajili ya fainali ya  kufuzu  fainali za Afrika kwa timu za vijana za U-17 (Afcon) yamepangwa kufanyika nchini mwezi Agosti jijini Dar es Salaam.

 

Nchi hizo ni Kenya, Uganda, Burundi, Sudan, Ethiopia, Rwanda  na Tanzania. Nchi ya nane katika mashindano hayo itapatikana katika mashindano madogo yatakayoshirikisha nchi za Sudani Kusini, Eritrea, Djiobuti na Somalia ambazo zitacheza hatua ya mtoano.

 

Tanzania kupitia Serengeti Boys inashiriki katika mashindano hayo kama sehemu ya maandalizi, kwani imekwisha fuzu kutokana na kuandaa mashindano hayo.

 

Rais wa Shirikisho la Kandanda Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema kuwa CAF imebadili mfumo wa kutafuta timu za kufuzu katika mashindano ya vijana ambapo awali, ulikuwa timu kutoka kanda tofauti zinacheza na kanda nyingine.

 

 

Karia alisema kuwa mfumo huo ulikuwa unaondoa uwakilishi kwa nchi za ukanda mbalimbali na baadala yake nchi za Kanda ya Kaskazini, Kusini na Magharibi kutawala mashindano hayo.

 

“Sasa mashindano yatafanyika kwa kanda, kwa mfano ukanda wa Afrika Mashariki wenye nchi 12, timu hizo zitacheza kutafuta timu moja ambayo itaungana na timu za kanda nyingine kucheza fainali, ni mfumo kama wa mashindano ya Chan, lakini unatofautiana na idadi ya timu na uendeshaji wa mashindano,” alisema Karia.

 

Alifafanua kuwa kwenye Chan, nchi  za kanda moja ucheza kwa mechi ya nyumbani na ugenini, lakini kwa upande wa vijana, nchi zinakutana katika nchi moja na kucheza kwa makundi mpaka kumpata mshindi.

“Ni mfumo mzuri kwani unaleta uwakilishi kwa kila kanda kama ilivyto katika Chan ambapo ukanda wa Cecafa uliwakilishwa na Rwanda na Sudan, tupo katika maandalizi mazuri, timu yetu itajiandaa na kutumia fursa hiyo, tunataka kushinda kombe na siyo kuandaa tu,” alisema.

Vurugu za mashabiki zasababisha kifo cha askari
Injili ya mchungaji yamtia mbaroni, ''...Wanawake chanzo cha matatizo duniani’'