Mtendaji mkuu wa mabingwa wa soka Tanzania bara Simba SC, Senzo Mazingiza amethibitisha kupokea ripoti ya kocha Sven Vanderbroeck kuhusu Usajili wa msimu ujao.

Kocha Sven amependekea hitaji la wachezaji 5 wa nguvu, ambapo kati hao wachezaji wa ndani na watatu wachezaji wa nje na kazi ya kutafuta wachezaji hao imeanza mara moja.

Katika ripoti hiyo Kocha Sven ameeleza kigezo cha umri na uwezo kitumike, haswa kuchagua wachezaji hao wachezaji wanaotakiwa ni mabeki watatu.

Wawili wa Kati na moja wa kulia, kiungo mkabaji mmoja na mshambuliaji mmoja. Senzo amesema wameanza kubainisha wachezaji hao kabla ya kuwachuja na kufanya Usajili.

“Tumeshaanza kulifanyia kazi pendekezo la kocha, kupitia ripoti aliyoiwasilisha kwangu, ninaamini kila hatua itakamilishwa kama inavyotarajiwa.”

“Lengo ni kuwa na kikosi bora na imara kwa msimu ujao wa ligi ya Tanzania bara, na michuano ya klabu bingwa Afrika, tunaamini sifa za wachezaji zilizopendekezwa na kocha, tutawapata na watakua sehemu ya kikosi chetu kwa msimu ujao.”

Simba ina nafasi kubwa ya kushiriki michuano ya klabu bingwa msimu ujao, kufuatia kuwa na mwenendo mzuri kwenye ligi ya Tanzania bara msimu huu. Mpaka sasa klabu hiyo kongwe nchini inaongoza msimamo wa ligi kwa kumiliki wa alama 71.

Wanajeshi wa Chad zaidi ya 90 wauawa na Boko Haram
Wananchi wa Marekani kutoka karantini kunusuru uchumi

Comments

comments