Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Avemaria Semakafu ametatua utata ulioibuka kuhusu kigezo cha umri wa mwanafunzi kujiunga na masomo ya Sekondari kidato cha tano na sita na kusema taarifa ambayo inasambaa imekuwa na makosa.

Semakafu amesema kuwa yametokea makosa ya kiuandishi, amefafanua ili kujiunga na masomo ya kidato cha tano na sita mwanafunzi anatakiwa kuwa na umri usiozidi miaka 25.

Na kusema taarifa iliyodai mwanafunzi kujiunga na kidato cha tano anatakiwa kuwa na umri usiozidi miaka 20, ni taarifa iliyochapishwa kimakosa, hivyo ameomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kufuatia taarifa hiyo.

“Kumetokea makosa ya kiandishi, miaka ni 25 ya kujiunga sekondari na sio 20 kama ambavyo inasomeka kwenye ile karatasi” amesema Semakafu.

Makosa ya kiuandishi yalifanyika katika barua ambapo kipengele E, Kimefafanua kuwa Mwanafunzi atakayedahiliwa asiwe na umri zaidi ya miaka 20.

Image result for Ukraine

Taarifa hiyo imefanyiwa marekebisho, barua mpya iliyochapishwa imeeleza ili kudahiliwa kujiunga na kidato cha tano na sita, Kipengele D kinasema mwanafunzi asiwe na umri zaidi ya miaka 25 na imesainiwa na Kaimu katibu Mkuu, Dkt. Ave Maria Semakafu.

 

 

Video: Kampuni ya DataVision International kufanya mambo makubwa mwaka 2018
Serikali yakanusha kufungia mitandao ya kijamii