Mbunge wa Jimbo la Rombo (CHADEMA) Joseph Selasini ameitaka serikali kutoa nafasi za ajira kwa vijana waliomaliza mafunzo katika Jeshi la la kujenga Taifa (JKT) ili kuepuka hatari ya vijana hao kujiingiza katika vitendo vya uhalifu baada ya kumaliza mafunzo.

Ameyasema hayo Bungeni wakati wa kuchangia hoja katika bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa na kuongeza kuwa serikali isipotoa ajira kwa vijana hao itapelekea hali ya usalama wa taifa kutetereka kwasababu vijana hao wana mafunzo kamili ya kijeshi.

“Kuna manung’uniko ya vijana kwamba wale waliomaliza JKT awamu ya nne, hawaja ajiliwa na hawanufaiki na utaratibu huu, sasa hawa ni vijana ambao wamefunzwa siraha, wakiachwa na manung’uniko mtaani tutakuja kutengeneza kitu kingine, hii inanipa hofu kama hatuwezi kuajiri vijana wote ni vizuri tukaangalia vijana ambao tunaweza kuwapa mafunzo ya kijeshi na wale ambao tunafikiria wataenda nyumbani wapewe mafunzo mengine, vinginevyo kuwafundisha kijeshi na kuwaacha mtaani italeta athari kubwa sana” amesema Selasini.

Aidha, Mbunge huyo ameongeza kuwa wanajeshi nchini wanapaswa kufanyiwa kipimo bora cha nidhamu yao kutokana na baadhi ya uwepo wa baadhi ya wanajeshi kufanya matukio ya kiuhalifu katika makazi ya wananchi.

Kwa upande mwingine Mbunge huyo amesema kwamba serikali inatakiwa kuwekeza nguvu kubwa katika Jeshi ikiwemo kutimiza mahitaji yote ya kifedha ili kuondoa fedheha ya jeshi kuwa na madeni kutokana na upungufu wa fedha unalolikabili Jeshi hilo.

Hata hivyo, Bunge kwasasa linajadili mapitio ya mapato na matumizi katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi kujenga Taifa katika mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo Waziri Dkt Hussein Mwinyi ameliomba Bunge kuizinisha kiasi cha shilingi trilioni 1.7 za wizara hiyo.

Video: Lulu azua mjadala nchini.., JWTZ yatakiwa isaidie Polisi kiintelijensia
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Mei 15, 2018