Saudi Arabia sasa imeamua kulegeza masharti yake kwa raia wa kigeni ambao si wanandoa ambapo sasa wanaruhusiwa kulala chumba kimoja cha hoteli tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo ilikuwa marufuku.

Mabadiliko hayo ni sehemu ya masharti ya kupata viza yaliyotangazwa hivi karibuni na taifa hilo ambalo limekuwa likiendeshwa na sheria za kihafidhina za dini ya Kiislamu.

Pia kwa sasa wanawake wataruhusiwa kupanga vyumba vya hoteli peke yao.

Mabadiliko hayo yanakuja katika kipindi ambacho serikali ya Saudia inajipanga kukuza sekta ya utalii nchini humo.

“Raia wote wa Saudia wanatakiwa kuonesha vitambulisho vya familia ama uthibitisho wa mahusiano wakati wa kukodi vyumba vya hoteli,” ameeleza Kamishna wa Utalii na Urithi wa Taifa wa Saudia katika taarifa yake.

“Uthibitisho huo hata hivyo hautawahusu watalii raia wa kigeni. Wanawake wote, wakiwemo raia wa Saudia sasa ruksa wanaweza kupanga vyumba vya hoteli wakiwa peke yao, ilimradi tu wawe na vitambulisho.”

Mabadiliko hayo yanaeleza kuwa watalii wanawake si lazima wavae ushungi lakini wanategemewa kuwa watavaa kwa kujihifadhi vizuri.

Waziri Mkuu amsweka ndani afisa aliyenunua vifaa vya ujenzi kwenye duka la nguo
Chanzo cha magari kuwaka moto safarini, Jeshi la Zima Moto laweka wazi