Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni (CHADEMA), Salum Mwalimu amesema kuwa sanduku la kupigia kura katika mtaa wa Idrisa Magomeni Jijini Dar es Salaam limeibiwa huku watu wakishuhudia kitendo hicho kikifanyika na hakuna hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na kituo kimoja cha televisheni kutoka katika kituo hicho baada ya kupata taarifa kutoka kwa mmoja wa wakala wake aliyempigia simu kumtaarifu kwamba kuna mtu ameiba sanduku la kupigia kura akiwa na gari na kutokomea kusikojulikana.

“Nimepigiwa simu na wakala wangu kuwa sanduku lilikuja na kuibwa lakini nikazungumza na msimamizi wa kituo hichi pamoja na Polisi ambaye ni msimamizi mkuu wote walikiri kuwa sanduku limeibwa na kwa pamoja wote tulikubaliana kuwa sanduku liliibiwa na mtu ambaye alikuja na kulipora japo watu walikuwa wamekaa hapa hapa akatokomea nalo,”amesema Mwalimu

Amesema kuwa baada ya dakika 10 sanduku hilo lilirudishwa, hivyo ameseishangaa Tume na jeshi la polisi kuruhusu kuendelea kwa uchaguzi huo.

Salum Mwalimu: Niko tayari kupoteza maisha kuliko kuibiwa kura

Hata hivyo, kwa upande wake, Wakala wa CHADEMA katika kituo hicho, Msafiri Mussa amesema waliona gari aina ‘Land Rover’ na kushuka mtu mmoja akiwa na askari kisha akachukua sanduku hilo na kutokomea nalo.

Kitakacho wakuta CUF wasimlaumu mtu- Kamanda Mambosasa
Tunataka haki itendeke Siha- Elvis