Mabingwa mara nne Afrika, Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wanatarajiwa kuja kuweka kambi fupi Dar es Salaam kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu hiyo yenye Watanzania wawili, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu itakuwa na mchezo mgumu wa ugenini dhidi ya Al Hilal nchini Sudan Jumapili ya Agosti 23, mwaka huu na kuelekea mechi hiyo itakuja kuweka kambi Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ameiambia amesema kwamba Mazembe wameomba kutumia Uwanja wa Azam FC kwa mazoezi.

Wanataka kuja kutumia vifaa vyetu kwa maandalizi kwa maana ya Uwanja wa mazoezi na vitu vingine ikiwemo gym. Kimsingi tumewakubalia na kuna uwezekano pia tukacheza nao mchezo wa kirafiki,”amesema Kawemba.

Kikosi cha Azam FC kipo kambini visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 22 dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC na kinaweza kurejea Dar es Salaam kucheza na Mazembe.

Haijajulikana kama Mazembe itakuwa tayari kucheza mechi zaidi za kujipima na vigogo wa hapa Simba na Yanga ambao nao wangependa changamoto hiyo.

Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Smouha ya Misri jana mjini Lubumbashi umeipandisha kileleni mwa Kundi A Mazembe Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Mazembe, bao pekee la TPM lilifungwa na Roger Assale dakika ya 53 na sasa mabingwa hao mara nne Afrika wanatimiza pointi nane baada ya kushinda mechi mbili na sare mbili.

Al Hilal inabaki na pointi zake tano baada ya juzi kufungwa 1-0 nyumbani na Moghreb Tetouan ya Morocco ambayo sasa nayo imefikisha pointi tano. Smouha ya Misri ina pointi tatu.

Babu Wenger Akataa Kumlaumu Cech
Profesa Lipumba Awajibu Ukawa, Asema Wamejichanganya