Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, leo anatarajiwa kuwa mgeni rasim kwenye uzinduzi wa mpango wa kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam,ambapo katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia,Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga amesema lengo kubwa la mpango huo ni kutokomeza ukatili wowote dhidi ya wanawake na watoto.

Nkinga amesema  Tanzania ni moja kati ya nchi nne za kwanza duniani na pekee Afrika iliyowezeshwa kupitia jukumu la kuwezesha nchi wanachama wa umoja wa mataifa (UN) kuandaa mpango huo.

“Lengo la mpango kazi huu ni kupunguza vitendo vya ukatili wa kimwili kwa wanawake wenye umri wa miaka 15 hadi 49 kutoka asilimia 39 hadi 10″amesema Nkinga.

Aidha, amesema kuwa malengo mengine ni kuongeza upatikanaji wa huduma rafiki kwa wahanga  wa ukatili kutoka vituo vinne hadi 26.

Hata hivyo amesema kuwa Mpango huo  utabainisha kazi zitakazotekelezwa na kila mdau kuanzia Familia, Jamii, Halmashauri, Mikoa, Wizara na Sekta binafsi.

#HapoKale
Bomberdie kuanza safari mashariki ya mbali