Baada ya Mbwana Samatta, kujiunga na timu ya Aston Villa inayoshiriki ligi kuu soka nchini Uingereza akitokea KRC GENK sasa macho ya wadau wengi wa soka yanasubiri kuona kama mchezaji huyo akicheza fainali dhidi ya Manchester United au Manchester City.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofa ya DSTV inayofahamika kama kitu juu ya kitu mkuu wa kitengo cha masoko cha Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo amesema kama Aston Villa wakifanikiwa kupita katika hatua ya nusu fainali ya kombe la Carabao basi watamsubiri mshindi baina ya Manchester United au Manchester City ili wacheze fainali ambapo itakua fursa kwa Samtta kucheza mchezo huo.

”Mbwana amejiunga na Aston Villa, watu wengi wanazungumzia Aston Villa iko chini kwenye msimamo wa ligi lakini hakuna mtu aliyezungumzia ipo kwenye nusu fainali ya ‘Carabao Cup’ na mechi ya kwanza Aston Villa akatoa droo ya 1-1 na mechi ya marudiano inafanyika mwezi huu ambapo Aston Villa atahitaji suluhu ili waende kucheza fainali maanake Samatta ana uwezekano wa kuwa bingwa wa kikombe uingereza,”amesema Shelukindo.

Samatta amejiunga na Villa akitokea katika timu ya KRC GENK ya nchini ubeligiji kwa ada ya paundi milioni 10 ambapo mkataba utamfanya kudumu katika timu hiyo kwa muda wa miaka minne na nusu.

Video: Kisa mzee Abdul kumuacha Bi Sandra, ''Sijawahi kujuta'', ''Sipendi hiki kwa Diamond''
Tanga yang'ara miradi kwa njia ya 'Force Account'

Comments

comments